MASHIRIKA YA KIJAMII YAMTAKA KUJUMUISHA MAAFISA WA KUKABILI MAJANGA KATIKA MAANDALIZI YA MADARAKA
Viongozi wa mashirika ya kijamii katika kaunti ya bungoma wamekosoa utayarifu wa kaunti katika kukabili majanga kufuatia visa vya hivi majuzi Wakati ambapo kaunti hiyo inaendeleza maandalizi ya sherehe za madaraka zitakazofanyika mwezi ujao.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari mjini Bungoma viongozi hao wakiongozwa na Lumumba Wekesa wamemtaka gavana wa kaunti hiyo Ken Lusaka kuwajumuisha maafisa wa kukabili majanga katika kaunti hiyo katika maandalizi hayo.
Vile vile viongozi hao wamesuta serikali ya kaunti kwa kununua basi la kaunti badala ya gari la zima moto licha ya wakaazi kupotez mali mara kwa mara kutokana na Mikasa ya moto.
Imetayarishwa na: Janice Marete.
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































