MWAURA ATETEA SERIKALI DHIDI YA KUFELI, MSWADA WA CHERARGEI
Kauli za viongozi wa kidini za kuikosoa serikali ya Kenya Kwanza zimeendelea kuibua shutuma kutoka kwa serikali hiyo, wa hivi punde akiwa msemaji wa serikali Isaac Mwaura ambaye amesema kuwa serikali imewajibika kwa kuwaajiri walimu na kupambana na ufisadi.
Akizungumza na wanahabari jijini Nairobi, Mwaura amesema kuwa serikali imefanikiwa kurejesha shilingi bilioni 28 kutoka kwa watuhumiwa wa ufisadi.
Aidha, amesema serikali imefanya kila juhudi kuimarisha uchumi na kulipa madeni.
Kuhusu mswada wa seneta wa Nandi Samson Cherargei kuongeza muhula wa Rais na viongozi wengine wanaochaguliwa kutoka miaka 5 hadi 7, Mwaura amekana kuhusika kwa serikali kwenye mswada huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































