DIDMUS- GACHAGUA ATAKUWA RAIA DISEMBA

Mbunge wa Kimilili kaunti ya Bungoma Didmus Barasa, amesema kwamba naibu rais Rigathi Gachagua atabanduliwa kutoka mamlakani kabla ya Disemba mwaka huu.
Akihutubu katika eneo bunge lake, Barasa amesema hatua ya kumbandua Gachagua imechochewa na uamuzi wake wa kueneza siasa za kikabila mwaka jana na kulifananisha taifa na kampuni ya wenye hisa.
Hata hivyo, wandani wa Gachagua wameapa kupinga hatua yoyote ya kumtimua.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa