#Sports

HATUMTAKI DIAZ WAEMA LIVERPOOL

Liverpool wamekataa ombi rasmi kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji Luis Diaz.

Mkurugenzi wa spoti wa Bayern Max Eberl amefahamishwa kuwa klabu hiyo ya Premier League haina nia ya kumuuza Diaz na haitaingia kwenye majadiliano ya mshambuliaji huyo.

Diaz, 28, alikabiliwa na hali kama hiyo kutoka kwa Barcelona mapema msimu jana lakini mabingwa hao wa Premier League pia walikataa.

Liverpool wamesisitiza kwamba Diaz hauzwi kwa bei yoyote msimu huu wa joto, kutokana na mchango wake muhimu katika timu hiyo tangu alipowasili kutoka Porto mwaka 2022.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia alifunga mabao 22 kwa klabu na nchi msimu uliopita huku akiibuka kama kiungo muhimu katika kikosi cha Arne Slot kilichoshinda taji.

Alifunga mabao 13 na kutoa asisti saba kwenye ligi huku Liverpool ikitwaa ubingwa kwa pointi 10.

Diaz, ambaye amebakiza miaka miwili kumaliza mkataba wake Anfield, alivutia Manchester City msimu uliopita wa joto na pia ana mashabiki nchini Saudi Arabia.

Liverpool wamethibitisha kuwa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Giovanni van Bronckhorst atajiunga na klabu hiyo kama kocha msaidizi wa meneja Arne Slot.

Van Bronckhorst anarithi mikoba ya John Heitinga, ambaye aliwaacha mabingwa hao wa Ligi Kuu na kuwa kocha mkuu wa Ajax.

Van Bronckhorst mwenye umri wa miaka 50, ambaye aliichezea Arsenal Ligi ya Premia, ameziongoza Rangers, Besiktas na Feyenoord.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HATUMTAKI DIAZ WAEMA LIVERPOOL

BAENA AJIUNGA NA ATLETICO MADRID

HATUMTAKI DIAZ WAEMA LIVERPOOL

BLOGA NDIANG’UI APATIKANA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *