MAFUTA ‘MABOVU’ YANAUZWA NCHINI- KEBS

Kuna uwezekano kwamba wakenya wanatumia mafuta ya kupika ambayo hayaafikii viwango hitajika vya ubora, baada ya kubainika kwamba takribani lita milioni 32 za mafuta hayo zilizoagizwa kutoka Indonesia, Malasya na Misri yalikuwa na dosari.
Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya viwanda na biashara katika bunge la seneti, mkurugenzi mkuu wa shirika la kutathmini ubora wa bidhaa KEBS Esther Ngari, amefichua kwamba mafuta hayo yanaendelea kuuzwa nchini licha ya shirika hilo kutilia shaka ubora wa mafuta hayo.
Kulingana naye, mafuta hayo hayajarejeshwa yalikotoka kutokana na uchunguzi, huku lita zingine milioni 20 zikisalia katika bandari ya Mombasa mwaka mmoja tangu kuwasili kwake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa