#uncategorized

RED CROSS YAWAOKOA WANNE WALIOANGUKIWA NA JENGO MATHARE

Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu wamewaokoa watu wanne kutoka kwenye vifusi vya jengo ambalo limeporomoka katika eneo la Kiamaiko, mtaani Mathare jijini Nairobi.

Watatu kati ya wanne hao wamepelekwa katika vituo vya afya vilivyo karibu, huku mmoja aliyekuwa na majeraha madogo akitibiwa katika eneo la mkasa.

Wakazi walioshuhudia tukio hilo wamesema zaidi ya watu 10 walikuwa wakisaka vyuma vikuu kuu kwenye jengo ambalo lilikuwa limeratibiwa kubomolewa kabla ya jengo hilo kuporomoka ghafla na kuwafunika.

Kwa sasa shughuli za uokoaji zinaendelea

EACC YAKANA KUTUMIWA KISIASA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *