OGAMBA: SHULE ZIMEPOKEA BILIONI 19
Ni afueni kwa shule za msingi na upili za umma baada ya shilingi bilioni 19 kati ya bilioni 48 kutolewa ili kufanikisha shughuli za masomo shuleni humo, kufuatia lalama za walimu wakuu.
Kwa mujibu wa waziri wa elimu Julius Ogamba, malimbikizi ya fedha hizo yatatolewa kufikia wiki ijayo.
Ameyasema haya alipokuwa akikagua madarasa ya gredi ya 9 eneo la Kikuyu kaunti ya Kiambu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































