#Local News

MARUFUKU YA MAHAKAMA KWA POLISI

Jaji wa Mahakama kuu Mugure Thande amewapiga marufuku maafisa wa polisi dhidi ya kutumia malori ya kurusha maji, vitoza machozi, risasi za chuma na zile za mipira au silaha zozote butu dhidi ya wanaofanya maandamano ya amani kupinga mswada wa fedha ambao umetupiliwa mbali.

Katika kesi iliyowasilishwa mahakamani humo na mkenya kwa jina Saitabao Ole Kanchory, jaji huyo aidha ameharamisha matumizi ya nguvu kupita kiasi au vurugu dhidi ya waandamanaji.

Aidha, mahakama imetoa amri ya kuwazuai maafisa wa polisi kutekeleza mauaji ya kiholela, kuwakamata, kuwateka nyara, kuwazuilia, kuwahangaisha, kuwatishia, kuwatesa au kuwadahalilisha waandamanaji kwa njia yoyote.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MARUFUKU YA MAHAKAMA KWA POLISI

SERIKALI KUIMARISHA EPZ

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *