YEIMBE ACHAGULIWA KUA REFARII MSAIDIZI WA MECHI YA KOMBE LA DUNIA KLABU

Mwamuzi wa Kenya Stephen Yiembe ameteuliwa kuwa refarii msaidizi wa pili wa mechi ya Kombe la Dunia la Klabu ya FIFA kati ya Real Madrid na RB Salzburg mnamo Ijumaa, Juni 27, Uwanja wa Lincoln Financial huko Philadelphia, Marekani, kuanzia saa 4:00 alfajiri EAT.
Mechi hiyo itasimamiwa na timu kubwa ya Waafrika, ikiongozwa na Beida Dahane wa Mauritania kama mwamuzi wa kati na Jeerson Santos wa Angola kama msaidizi wa kwanza. Ning Ma wa China atakuwa mwamuzi wa akiba.
Hili ni jukumu la hali ya juu zaidi la Yiembe katika kazi yake ya urefarii ya muongo mzima.
Refa huyo mzaliwa wa Nakuru ameongoza michezo ya Olimpiki ya 2024 na nusu-fainali ya CAF Champions League.
Pia aliongoza mechi ya Inter Milan dhidi ya Urawa Red Diamonds mapema kwenye michuano hiyo ya kombe la dunia la vilabu
Imetayrishwa na Nelson Andati