KENYA YASHUKA DIMBANI NA ARGETINA

Kinyang’anyiro Cha Cha Kuwania Taji La Mchezo Wa Raga Ya Wachezaji Saba Saba Katika Olimpiki Ya 2024 Kinaanza Leo Huku Mabingwa Wa Afrika Kenya Wakikabiliana Na Mshindi Wa Pili Wa HSBC Sevens Na Mabingwa Wa Mfululizo Wa Raga Ya Dunia Argentina Katika Mechi Yao Ya Ufunguzi Ya Kundi “B” Katika Uwanja Wa Stade De France Saa Kumi Na Moja Jioni Kwa Saa Za Kenya Kabla Ya Muogeleaji Ridhwani Abubakar Na Malkia Wa ‘Fencing’ Alexandra Ndolo Kuingia Uwanjani Siku Ya Jumamosi.
Kulingana Na Kocha Wa Timu Ya Shujaa Kevin Wambua, Timu Hiyo Imejitayarisha Vilivyo Kwa Ajili Ya Kazi Iliyo Mbele Yao Ikiwa Imefanya Mazoezi Makali Nchini Kenya Na Miramas.
Hii Itakuwa Mara Ya Tatu Kwa Kenya Kushiriki Katika Michezo Hiyo Ikishindwa Kufuzu Kwa Robo Fainali Katika Michuano Ya Olimpiki Ya Rio Na Tokyo. Herman Humwa Na Vincent Onyala Walikuwa Sehemu Ya Timu Iliyomaliza Ya 9 Katika Makala Ya Mwisho Ya Michezo Ya Olimpiki Ambapo Kenya Ilishinda Michezo Miwili Dhidi Ya Japan Na Ireland Na Sasa Wanatumai Wao Uzoefu Utawasaidia Wachezaji Chipukizi.
Shujaa Itamenyana Na Miamba Wengine Australia Leo Saa Mbili Usiku Na Kumaliza Mechi Zao Za Makundi Dhidi Ya Samoa Siku Ya Alhamisi Kuanzia Saa Tisa Alasiri.
Michuano Ya Raga Ya Wachezaji Saba Na Mechi Za Soka Zinaanza Leo Kabla Ya Hafla Ya Ufunguzi Rasmi Siku Ya Ijumaa.
Imetayarishwa na Nelson Andati