WAUGUZI BUNGOMA WAANZA MGOMO, WAWATAKA WAGONJWA WAONDOKE
Baadhi ya wakazi katika kaunti ya Bungoma wametatizika kupata huduma za kimatibabu katika vituo vya umma kwenye kaunti hiyo kufuatia mgomo wa wauguzi wanaolalamikia madai ya kutotekelezwa kwa mkataba wao.
Wakizungumza mjini Bungoma, wauguzi hao wamelalamikia mazingira duni ya kazi, wakishikilia kwamba hawatarejea kazini hadi malalamishi yao yatakapoangaziwa.
Miongoni mwa matakwa yao ni ajira ya kudumu na nyongeza ya mshahara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































