MADAKTARI KUTRH WAGOMA, WATATIZA MATIBABU

Shughuli za matibabu katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta zimesambaratika kufuatia mgomo wa madaktari hospitalini humo ambao umeanza hii leo.
Madaktari hao wanalalamikia kusitishwa kwa bima ya afya na kile wanachokitaja kuwa usimamizi mbaya wa hospitali hiyo, na kutishia kusitisha huduma zote iwapo malalamishi yao hayataangaziwa.
Kulingana nao, kaimu afisa mkuu Isaac Kamau ndicho chanzo cha masaibu yao, na hivyo anafaa kutimuliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa