GACHAGUA AKANA KUJIUNGA NA CHAMA KIPYA
Naibu Rais Rigathi Gachagua amejitenga na taarifa kwamba amepata chama kipya cha kisiasa, akizitaja taarifa hizo kuwa za uongo na zenye nia mbaya.
Kwa mujibu wa gazeti moja nchini hii leo, Gachagua yuko kwenye mchakato wa kujiunga na chama cha The New Democrats kufuatia mgawanyiko wake na Rais William Ruto.
Hata hivyo, Gachagua amelishutumu gazeti hilo, akisema hatua hiyo inalenga kumdhalilisha kama Naibu rais na naibu kinara wa chama tawala cha UDA.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































