BONIFACE MWANGI, WENZAKE WAPEWA DHAMANA

Mwanaharakati Boniface Mwangi na washtakiwa wenza wanne wameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi elfu 20 kila mmoja baada ya mahakama ya Milimani kudinda kutoa amri ya kuwazuilia kwa siku 21 jinsi upande wa mashtaka ulivyokuwa umeomba.
Watano hao walikamatwa hapo jana katikati mwa jiji nla Nairobi walipokuwa wakiandamana kuadhimisha mwezi mmoja tangu maafa yalipotokea katika majengo ya bunge baada ya waandamanaji kuingia kwa lazima.
Idara ya upelelezi DCI imetaka wazuiliwe kwa siku 21 ili kukamilisha uchunguzi dhidi yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa