WAHADHIRI, SERIKALI WAKOSA MWAFAKA

Shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma zimeendelea kuathirika kwa wiki ya 4 huku wahadhiri wakiitaka serikali iwape shilingi bilioni 9.7 za mishahara na marupurupu yao la sivyo waendelee na mgomo wao.
Wakiongozwa na katibu wa muungano wa UASU Dakta Constantine Wasonga, wahadhiri wamesema mgomo ungalipo licha ya serikali kutoa shilingi bilioni 4.3.
Hata hivyo, mazungumzo baina ya serikali na wahadhiri hao yamegonga mwamba, wahadhiri wakishinikiza kutekelezwa kikamilifu kwa makubaliano yao.
Wakati uo huo, Wasonga ameitaka serikali kuwaajiri wafanyakazi Zaidi wa vyuo vikuu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa