WAKAZI NAIROBI WAANDAMANA KUMSHUTUMU GAVANA

Wakazi jijini Nairobi wameandamana hadi katika afisi ya gavana Johnson Sakaja wakilalamikia ubomozi na kuhamishwa kwa lazima, zoezi wanalohoji linafanyika kwa ubaguzi.
Wakazi hao aidha wamelalamikia hatua ya ujenzi kufanyika kiholela na manedeleo yasiyopangiwa.
Hata hivyo, maandamano hayo yaliyoanzia katika eneo la Jeevanjee hadi katika bunge la kaunti na lile la kitaifa, yametibuliwa baada ya makundi pinzani kukabiliana.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































