AMUUA JIRANI KWA MADAI YA KUMWITA BABAYE MCHAWI

Polisi katika eneo la nyakatch kaunti ya Kisumu wamemkamata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 baada ya kudaiwa kumuua Jirani yake kufuatia madai ya kumwita babaye mchawi
Babake mshukiwa ayejulikana kwa jina Valentine Ochieng aliuliwa badae na umma uliojawa na ghadhabu na nyumba nne pia zinazodaiwa kuwa za mshukiwa pia ziliteketezwa
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya nyabondo baada ya kuhamishwa katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga
Polisi wameanzisha uchunguzi kufuatia kisa hicho