#Football #Sports

HUSSEIN AZINDUA AZMA YAKE YA KUWANIA URAIS WA FKF

Makamu mwenyekiti wa Murang’a Seal Hussein Mohamed ametangaza rasmi kuwania kiti cha urais wa Shirikisho la Soka la Kenya FKF, huku uchaguzi ukipangwa kufanyika Disemba.

Wakati wa hotuba jana Jumatano, Hussein alitoa notisi kwa uongozi wa sasa, akiwaambia wajiandae kuondoka ofisini.

Alisema nchi ina uwezo mkubwa wa kupata ukuu, kutokana na kundi kubwa la vipaji vinavyoweza kutumiwa.

Hussein aliwaomba wajumbe kujitokeza kwa ujasiri na kuokoa soka la Kenya kutoka kwenye taya za watu wanaojitafutia wenyewe ambao wameharibu mazingira ya soka

Sehemu ya mpango wake ni kuhakikisha miundombinu ya kutosha inawekwa.

Amewahakikishia wafuasi wake ushindi, na kuongeza kuwa wamepata mafunzo muhimu kutoka kwa chaguzi zilizopita ambazo wangetumia kuwashinda wapinzani wao.

Imetayarishwa na Janice Marete

HUSSEIN AZINDUA AZMA YAKE YA KUWANIA URAIS WA FKF

ISHARA YA DHAHABU YA ALAMISI KATIKA MBIO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *