KINDIKI ATETEA ‘UCHUNGU’ WA SUKARI
Huku hayo yakijiri, naibu Rais Kithure Kindiki ametetea mageuzi yaliyofanywa katika sekta ya kilimo cha miwa ikiwemo kukodishwa kwa viwanda 4 vya kusaka miwa kuwa mojawapo ya mikakati ya kuimarisha sekta hiyo.
Ameyasema haya baada ya kupokea ripoti kuhusu sekta ya sukari, akitolea mfano wa kiwanda cha Mumias anachosema tayari matunda ya kukodishwa kwake yameanza kuonekana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































