AJIUA BAADA YA KUUA
Polisi katika Kaunti Ndogo ya Nyatike wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mvulana wa umri wa miaka mitatu anayedaiwa kuuawa na babake, ambaye kisha alifariki kwa kujitoa mhanga huko Magungu, Kaunti ya Migori.
Akithibitisha kisa hicho naibu wa Chifu eneo hilo Zacheus Odero amesema uchunguzi wao wa awali umethibitisha kuwa mvulana huyo alichapwa viboko na babake wakati wa pambano lililozuka kati yake na mamake.
Alipogundua kuwa amemuua mwanawe, mtu huyo alijinyonga ndani ya nyumba.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































