MKUTANO WA KILELE WA UWEKEZAJI NYANZA WAAHIRISHWA

Kongamano la kimataifa la uwekezaji la Nyanza lililokuwa likitarajiwa kufanyika kuanzia Ijumaa limeahirishwa.
Waandalizi wa hafla hiyo ya kikanda wanasema imepangwa upya ili kukabiliana na hali ya sasa nchini
Tarehe mpya ya kongamano hilo itatangazwa baadaye.
Rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga walitarajiwa kuhudhuria mkutano huo uliolenga kuwaleta pamoja wataalamu mbalimbali kutoka kaunti za Kisii, Nyamira, Homa Bay, Migori, Kisumu na Siaya.
Imetayarishwa na Janice Marete