PIGO KWA POLISI KESI YA LSK KUENDELEA
Ni pigo kwa polisi baada ya Mahakama Kuu kukataa ombi lao la kufutilia mbali kesi ya chama cha wanasheria nchini LSK kuhusu madai ya ukiukaji wa maadili wakati wa maandamano ya mwaka jana.
Jaji Lawrence Mugambi ameamua kuwa taratibu za ndani haziwezi kushughulikia ukiukaji wa haki za kimsingi.
LSK inataka maafisa wawajibishwe kwa kifo cha Rex Masai na Inspekta Jenerali azuiwe kuwatuma polisi wa kiraia kudhibiti maandamano.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































