#uncategorized

WALIMU WA JSS WAANDAMANA KOTE NCHINI

Masomo katika shule za sekondari ya msingi JSS yameendelea kulemazwa kufuatia maandamano ya walimu kushinikiza tume ya huduma za walimu nchini TSC  kuwaajiri kwa kandarasi za kudumu.

Walimu hao ambao walifanya maandamano jana jumatatu katika kaunti mbali mbali nchini walikosa kurejea kazini wanafunzi wakisalia kwenye njia panda.

Maandamano haya yuanajiri wakati ambapo mahakama ya leba imetoa agizo la kusitishwa kwa mgomo huo hadi pale kesi iliyowasilishwa na tume ya huduma za walimu TSC itakaposkilizwa na kuamuliwa.

Kulingana na TSC haina fedha za kufanikisha kandarasi za kudumu ikiomba muda Zaidi hadi agosti mwaka huu baada ya seriksli kuipa mgao zaidi.

NAIBU GAVANA WA KISUMU MATHEW OCHIENG OWILI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *