MLINZI AUAWA KATIKA UVAMIZI WA SHULE MAI MAHIU

Maafisa wa upelelezi wanasaka genge lililovamia shule moja eneo la Mai Mahiu kaunti ya Nakuru na kumuua mlinzi wa usiku.
Kwa mujibu wa polisi Mlinzi huyo kwa jina Boaz Orono amefariki dunia baada ya majeraha alipowasili katika Hospitali ya moja eneo hilo.
Genge hilo lilivamia shule hiyo na kumfunga mlinzi aliyekuwa zamu katika duka baada ya kumdunga kisu mara tatu kichwani kabla ya kufululiza katika duka la shule na kuiba magunia matatu ya mchele na sukari na baadae kuvamia nyumba ya mwalimu na kuiba kitapakalishi na simu ya mkononi.
Polisi walisema kuwa genge hilo lilitoroka baada ya kutekeleza wizi huo na kumwacha mlinzi huyo akivuja damu hatua iliyosababisha kifo chake.
Mwili huo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo ukisubiri uchunguzi wa maiti na taratibu nyinginezo.
Imetayarishwa na Janice Marete