#Local News

GACHAGUA NA WANDANI WA RUTO WATOFAUTIANA KISIASA

Dalili za mgawanyiko baina ya naibu wa rais Rigathi Gachagua na wandani wa rais William Ruto zinaendelea kuchipuka huku madai ya njama zaidi ya kumuhujumu Gachagua yakiibuliwa.

Katika madai ya hivi punde seneta wa Kirinyaga Kamau Murango ametaja njama ya kupunguza bajeti ya ofisi naibu wa rais na shughuli zake kwa asilimia 25.

Kulingana na Murango bajeti hiyo inapunguzwa kupitia kuondolewa au kupunguzwa kwa bajeti ya idara ambazo Gachagua anasimamia kama vile Kilimo.

Vile vile amedai kwamba bajeti ya shilingi milioni 70 ya kukabili konokono katika mashamba ya mpunga eneo la mwea imeondolewa huku bajeti ya kushughulikia mageuzi ya sekta ya kahawa haijajumuishwa katika makadiro ya bajeti ya mwaka wa 2024-2025 japo serikali imesema kwamba itajumuishwa katika bajeti ya ziada.

Wandani wa Gachagua wanamlaumu mwenyekiti wa bajeti Ndindi Nyoro kwa kutumia mamlaka yake visivyo ili kumuhujumu Gachagua.

Hata hivyo hapo jana baadhi ya wandani wa rais Ruto wakiongozwa na mbunge wa Kapsabet Oscar Sudi walimfokea Gachagua na kusema kwamba hawataruhusu viongozi kuwekewa mipaka kimaeneo na kikabila katika siasa zao.

Imetayarishwa na Janice Marete

GACHAGUA NA WANDANI WA RUTO WATOFAUTIANA KISIASA

ZIARA YA GACHAGUA BONDE LA UFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *