ANC YAPINGA TAARIFA ZA KUVUNJWA

Mwenyekiti wa chama cha ANC Kevin Lunami amepinga taarifa kwamba kuna mpango wa kukivunja chama hicho na kujiunga na UDA kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Lunami amesema ushirikiano uliopo baina ya chama hicho na serikali haimaanishi kuvunjwa kwa chama hicho, kauli yake ikiwiana na ya Katibu Mkuu wa chama hicho Omboko Milemba.
Hata hivyo, taarifa zinaashiria kuwa baraza kuu la ANC limeidhinisha kuvunjwa kwa chama hicho.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa.
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































