RAIS RUTO APINGA KESI ZA GACHAGUA

Hatma ya naibu rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua imechukua mkondo mpya, baada ya Rais William Ruto kuwasilisha kesi mahakamani akisema kuwa mahakama kuu haina mamlaka ya kusikiliza kesi zinazopinga kutimuliwa kwa Gachagua.
Kupitia wakili wake Adrian Kamotho, Rais amepinga kesi iliyowasilishwa na David Mathenge na wengine 4 katika mahakama kuu ya Kerugoya, Rais akisema ni mahakama ya upeo pekee ndio yenye uwezo wa kusikiliza kesi hizo.
Haya yanajiri wakati ambapo Gachagua anasubiri kusikilizwa kwa kesi hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa