WANAFUNZI WAVAMIA HELB KUDAI MIKOPO
Athari za kucheleweshwa kwa mikopo ya bodi ya kufadhili elimu ya juu HELB zimeanza kujitokeza, baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wakivamia afisi za bodi hiyo kushinikiza mikopo hiyo kutumwa.
Wanafunzi hao ambao wamekita kambi nje ya jumba la Anniversary Towers kwa muda, wamelalamikia kushindwa kufadhili masomo yao kutokana na ukosefu wa fedha.
Hata hivyo, bodi hiyo imeahidi kutoa fedha hizo kufikia mwisho wa siku ya leo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































