#Football #Sports

SITUMA ATOA WITO KWA GOR NA AFC KUTAFUTA SULUHU

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Kenya James Situma ametoa wito kwa Gor Mahia na AFC Leopards kutatua haraka masuala yao ya kiufundi na usimamizi, ili kurejesha makali yao ya ushindani ndani ya nchi.

Timu zote mbili zimepata tabu katika mechi zao za hivi majuzi na kwa mujibu wa Situma, yote yanatokana na tofauti za benchi la ufundi na usimamizi.

Gor ambao ni mabingwa watetezi wako nafasi ya 11 kwenye ligi huku Leopards wakiwa nafasi ya saba, na mashabiki wao wameandamana katika mechi za hivi majuzi wakidai matokeo bora.

Situma amesisitiza umuhimu wa kusuluhisha masuala yao kabla ya Mashemeji derby inayotarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

SITUMA ATOA WITO KWA GOR NA AFC KUTAFUTA SULUHU

KARANI MPYA WA KAUNTI YA HOMA BAY

SITUMA ATOA WITO KWA GOR NA AFC KUTAFUTA SULUHU

LEE AWAITA WACHEZAJI WAWILI KIKOSINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *