#Sports

ONYANGO AONDOKA STELLENBOSCH

Beki wa kimataifa wa Kenya Brian Onyango yuko mbioni tena kutafuta klabu mpya baada ya kumalizika kwa muda wake katika klabu hiyo ya Afrika Kusini.

Onyango alijiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu wa 2024-25 na aliweza kucheza mechi nane pekee katika michuano yote, na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali ya MTN8 na kufuzu kwa Kombe la Shirikisho la CAF.

Akiwa Cape Winelands mlinzi huyo nguli pia alirejea katika kikosi cha timu ya taifa kwa mara ya kwanza katika takriban miaka miwili na akawa mchezaji wa tatu ambaye si Mwafrika Kusini kuiwakilisha nchi yake alipokuwa mchezaji wa Stellenbosch.

Licha ya ufupi wa kukaa kwake katika klabu hiyo, ushawishi wake mkubwa ulimwezesha kuteuliwa kuwania tuzo ya SFC ya 2024-25 kwa ajili ya huduma yake ya mchezaji wa Stellenbosch. kwa klabu na kumtakia kila la kheri anapoanza sura inayofuata ya maisha yake ya soka,” klabu hiyo ilisema katika taarifa yao rasmi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Posta Rangers na Tusker FC sasa atatafuta klabu ambayo itampa muda wa kucheza huku akitarajia kuhifadhi nafasi yake katika timu ya taifa.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ONYANGO AONDOKA STELLENBOSCH

DONDOO ZA UHAMISHO EPL

ONYANGO AONDOKA STELLENBOSCH

GOFU YA KENYA YAIMARIKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *