ULINZI WALINDA KOMBE LA FKF

Ulinzi Starlets wameandikisha historia kwa kuwalaza Kibera Soccer Ladies 2-1 na kufanikiwa kutetea taji lao la Kombe la Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) na kuwa washindi wa kipekee mara tatu katika mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Police Sacco, Nairobi.
Ulinzi Starlets walionyesha nia mapema kwenye mechi hiyo, baada ya Nahodha Sheryl Andiba kufunga bao lao la kwanza dakika ya tano.
Wanajeshi hao hata hivyo walizawadiwa bao lao la pili dakika ya 40 kupitia kwa Lynda Kihara, na kupelekea Ulinzi kwenda mapumziko wakiwa na bao la kuongoza.
Kocha wa Ulinzi, Joseph Wambua Mwanza alisifu kikosi chake kwa kushikilia uongozi licha ya kutishwa na wapinzani kipindi cha pili.
Kwa upande wake, kocha wa Kibera Soccer Ladies David Vijago alihusisha kushindwa kwa timu hiyo mpya ambayo ilikuwa bado haijaimarika
Imetayarishwa na Nelson Andati