KAUNTI YA MIGORI YAZINDUA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WAZEE WASIOJIWEZA

Serikali ya kaunti ya Migori imeanzisha mpango wa kusajili na kulipia bima ya afya kwa wazee wasiojiweza ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi.
Afisa mkuu wa huduma za matibabu wa Kaunti ya Migori, Samwel Atula, amesema Idara ya Afya ya Kaunti hiyo inashirikiana kwa karibu na Idara ya huduma za kijamii kuwatambua wazee watakaosaidiwa kupata bima ya afya.
Atula aidha ameongeza kuwa wazee wengi wamekuwa wakikumbwa na changamoto za kupata huduma za afya.
Kauli yake imeungwa mkono na Peter Otianga, akiongeza kuwa kuna wazee wengi katika jamii wanaohitaji msaada kama huo na huku akitoa wito kwa wanajamii kujitokeza na kuwasaidia wahitaji.
Otianga pia ametoa wito kwa serikali kuu kuhakikisha kuwa wazee wote wanaostahili wanajumuishwa kwenye mpango wa utoaji wa pesa taslimu.
Imetayarishwa na Janice Marete