WAFANYABIASHARA GIKOMBA WASHTAKI SERIKALI YA NAIROBI
Wafanyabiashara katika soko la Gikomba jijini Nairobi wameelekea mahakamani wakitaka ubomoaji wa maeneo yao ya biashara kusitishwa
Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, ubomoaji huo umelemaza shughuli za biashara na hivyo kuathiri Maisha yao ya kila siku.
Aidha, wamesema kuwa wenzao wawili wamefariki kutokana na mzongo wa mawazo.
Mahakama itatoa uamuzi kuhusu suala hilo tarehe 10 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































