#Local News

WAKAZI WA ASHABITO KUNUFAIKA NA HUDUMA MPYA ZA UMMA

Wakazi wa kaunti ndogo ya Ashabito, kaunti ya Mandera, sasa wataanza rasmi kupokea huduma za umma karibu nao kufuatia uzinduzi wa rasmi wa huduma hizo na serikali, Hafla iliyoongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, ambaye ameahidi kuanzishwa kwa kituo cha Huduma Center katika mji wa Rhamu, kitakachohudumia wakazi wa Ashabito na Mandera Kaskazini kwa ujumla.

Uzinduzi huo umeambatana na utekelezaji wa mpango wa Huduma Smart Serikalini (Mandera Edition) unaolenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa maeneo ya mbali.

Vilevile, ofisi za serikali zimefunguliwa rasmi katika Ashabito, na msaada wa chakula uliotolewa kwa jamii.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *