GOR MAHIA WATOKA SARE

Mabingwa watetezi Gor Mahia walitoka sare tasa na vinara KCB katika uwanja wa Dandora huku mabingwa wa zamani Tusker wakicheza na Ulinzi Stars kwa sare ya 1-1 uwanjani Police Sacco.
Katika mechi nyinginezo, bao la Humphrey Obina kipindi cha pili liliipa Murang’a SEAL ushindi wa 1-0 dhidi ya AFC Leopards uwanjani St. Sebastian Park Arena.
Nao Police FC walipata ushindi wao wa kwanza msimu huu wa 2-0 dhidi ya Mathare United katika uwanja wa Police Sacco.
Bandari FC ilinyimwa nafasi ya kusonga mbele katika nafasi nne za juu baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Talanta katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.
KCB ambayo haijashindwa inaongoza ligi kwa pointi 14, tatu nyuma ya Kariobangi Sharks iliyo nafasi ya pili baada ya raundi sita.
Kwengineko walio mkiani Nairobi City Stars wakilala 2-0 uwanjani Mumias Complex dhidi ya Kakamega Homeboyz, ambao waliibuka na ushindi baada ya kushindwa mara mbili mfululizo.
Oliver Majak alifunga bao dakika ya sita kabla ya kipa wa Homeboyz James Ssetuba kupangua penalti ya Yuto Kusaba katika dakika ya 10.
Moses Shumah alifunga bao la pili dakika ya 45.
Imetayarishwa na Nelson Andati