KARUA: SERIKALI INA KIKOSI CHA KUTEKA WATU
Kiongozi wa chama cha NAC Kenya Martha Karua ameibua madai kwamba kuna kikosi maalum cha utekaji nyara na mauaji kinachofanya kazi kwa mamlaka ya serikali ili kukandamiza uhuru na haki za kujieleza kwa binadamu.
Kwa mujibu wa Karua kikosi hicho kinachojumuisha maafisa wa jeshi kutoka mataifa mbali mbali kinafanya kazi chini ya maagizo ya kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali..
Karua aidha ameishutumu serikali kwa kuanzisha kikosi hicho kwa lengo la kuwanyamazisha wanaokosoa serikali kwa kuwa kulingana naye hatua hiyo ni kinyume cha sheria za taifa hili.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































