GACHAGUA AKANA MASHTAKA YOTE 11

Hoja ya kutimuliwa kutoka afisini naibu rais Rigathi Gachagua itasikilizwa na bunge zima la seneti baada ya naibu huyo wa rais kukana mashtaka yote 11 mbele ya bunge hilo.
Miongoni mwa tuhuma dhidi yake ni ukiukaji wa katiba, utumizi mbaya wa afisi yake na utovu wa maadili.
Tuhuma hizo zimesomwa na karani wa bunge la seneti Jeremiah Nyegenye, huku Gachagua akikana kuhusika na tuhuma hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa