“POMBE YA MAUTI NA JELA”

Mahakama Kuu mjini Eldoret imewahukumu wafanyakazi wawili kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kuhusika na mauaji ya kikatili ya mfanyakazi mwenzao wakati wa unywaji wa pombe.
Walipofikishwa mbele ya Jaji Reuben Nyakundi, wawili hao, Daniel Kiprotich na Meshack Kipchirchir, wamepatikana na hatia ya kumuua Nicholas Tenai mnamo Septemba 28, 2019, katika kituo cha biashara cha Baharini, Turbo, Kaunti ya Uasin Gishu.
Jaji Nyakundi amesema upande wa mashtaka umethibitisha kesi yake dhidi ya washitakiwa hao bila shaka yoyote.
Mahakama imeelezwa kuwa wawili hao walimshambulia mfanyakazi mwenzao wakati wa unywaji pombe ambapo alifariki dunia siku nne baadaye Hospitali alipokuwa akipokea.
Kulingana na Afisa wa Uchunguzi (IO) Simon Wanjala, marehemu aliwaeleza wenzake kuwa alikuwa na shilingi 200 tu na kwamba baada ya kulipa deni lake, angebaki na shilingi 170 za kununua chakula kwa familia yake.
Wanjala amesema ugomvi ulizuka kati ya marehemu na wawili hao, baada ya hapo walimzingira wakati akielekea nyumbani na kumpiga.
Imetayarishwa na Janice Marete