PARENO, KARUGU WAHOJIWA
Kamati ya ulinzi na masuala ya kigeni katika bunge la kitaifa imewahoji Daktari Caroline Karugu na Judith Pareno walioteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu kama katibu mkuu kwenye wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na idara ya haki na masuala ya kikatiba mtawalia.
Daktari Karungu ametakiwa kuzungumzia uchaguzi wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC naye Pareno akitakiwa kutoa mtazamo wake kuhusu serikali ya muungano na utendakazi wake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































