KWA NINI OMBI LA RAILA LA KUGOMBEA WADHIFA WA MWENYEKITI WA AUC BADO HALIJAWASILISHWA?

Ombi la kinara wa upinzani Raila Odinga kuwania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) bado halijawasilishwa kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao.
Katibu Mkuu wa Masuala ya Kigeni Korir Sing’oei amesema kwamba ombi la Raila bado halijawasilishwa kutokana na machafuko na mkanganyiko ambao umekumba nchini katika muda wa wiki mbili zilizopita.
Uwasilishaji wa stakabadhi za Raila katika afisi za Umoja wa Afrika ulipangwa Juni 30.
Imetayarishwa na Janice Marete