#Sports

MWAMKO MPYA WA AFC LEOPARDS

Klabu ya AFC Leopards imepata mwamko mpya kupitia uongozi wa mchezaji wa zamani wa Harambee Stars Boniface Ambani, aliyechaguliwa hapo jana kuwa mwenyekiti wake, akiapa kuleta mageuzi katika usimamizi na uendeleshaji wa klabu hiyo.

Ambani alijizolea kura 1,101, na kumbwaga Enos Mutoka aliyepata kura 682, Ambani akichukua hatamu za uongozi kutoka kwa mwenyekiti anayeondoka Dan Shikanda.

Kwenye kampeni zake, Ambani aliahidi mageuzi kadhaa ikiwemo uwajibikaji, mageuzi ya kifedha, uboreshaji wa miundomsingi na ushirikishwaji wa mashabiki.

Wakati uo huo, Isaac Mulindi alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Leopards, huku Newton Lime akishinda uchaguzi wa mwekahazina.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWAMKO MPYA WA AFC LEOPARDS

MAPEPO YA NHIF YAIHANGAISHA SHA

MWAMKO MPYA WA AFC LEOPARDS

NAIROBI UNITED WAINGIA AFRIKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *