WAKAZI WA NAMWELA WAPOKEA UFADHILI WA MBUZI
Ni afueni kwa wakazi wa wadi ya Namwela kaunti ya Bungoma, baada ya kupokezwa mbuzi wa maziwa kutoka kwa mwakilishi wa wadi hiyo Charles Nangulu, ambaye amesisitiza kuwa ufigaji na kilimo ndio njia mwafaka ya kuboresha uchumi wao.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, mwakilishi wadi huyo amewahimiza walionufaika kuwatuza mifugo hao kama njia mojawapo ya kuondoa umaskini eneo hilo, walionufaika wakionyesha matumaini ya kuimarika kiuchumi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































