UPINZANI KUKAMILISHA ZIARA YA MAGHARIBI

Viongozi wa upinzani wameratibiwa kukamilisha ziara yao ya siku 2 katika eneo la Magharibi mwa nchi hii leo, ambako wamekuwa wakiwataka wakazi wa eneo hilo kuwaunga mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Miongoni mwa viongozi hao ni Rigathi Gachagua wa DCP, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Eugene Wamalwa wa DAP-K na aliyekuwa waziri wa usalama Fred Matiang’i, wanaosisitiza kuhakikisha kuwa Rais William Ruto hapati muhula wa pili.
Wamewataka wakazi kuungana ili kuleta mabadiliko uongozini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa