#Local News

UN YAONYA MZOZO WA SUDAN KUINGIA KWA MAJIRANI

Idadi ya watu waliotoroka nchini Sudan tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 2023 imezidi milioni 4, shirika la umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi likisema kuwa wengi wa wahanga wa vita hivyo walikabiliwa na uhabawa makazi.

Kwenye kikao na wanahabari jijini Geneva, nchini Uswizi, msemaji wa shirika hilo Eujin Byun, amesema iwapo makabiliano hayo yataendelea, huenda maelfu zaidi ya raia wakakimbia Sudan na hivyo kuyumbisha usalama wa kimaeneo na ulimwenguni.

Tayari wakimbizi zaidi ya 800 wamewasili katika taifa jirani la Chad, ambako wanakabiliwa changamoto za makazi kutokana na uhaba wa fedha.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UN YAONYA MZOZO WA SUDAN KUINGIA KWA MAJIRANI

HESHIMA IDUMU KWA WANYAMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *