MASSIMILIANO AIAGA JUVENTUS
Kilabu cha Juventus kimessema wamefikia makubaliano na kocha Massimiliano Allegri, ambaye walimfukuza wiki mbili zilizopita, ili kumaliza mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 56 alifukuzwa kazi mnamo Mei 17 baada ya kulipuka kwa hasira wakati wa ushindi wa fainali ya Kombe la Italia dhidi ya Atalanta siku mbili zilizopita.
Siku ya Jumatatu klabu hiyo ilisema pande hizo mbili zilikubaliana masharti ya kutengana.
Juve walishinda Kombe lao la 15 la Italia mnamo Mei 15 lakini Allegri alipandwa na hasira, kwanza alitolewa kwa kadi nyekundu dakika za mwisho baada ya kuwazomea wasimamizi wa mechi na kisha kuwapungia mkono.
Juve walimaliza wa tatu kwenye jedwali la Serie A, pointi 23 chini ya washindi Inter Milan.
Allegri aliisaidia Juve kutwaa mataji 12 katika misimu miwili na alikuwa na kandarasi hadi 2025.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































