RUTO AZUNGUMZIA MADENI VYUONI
Rais William Ruto amehimiza ushirikiano miongoni mwa washikadau wa elimu ili kuvikwamua vyuo vikuu vya umma kutoka kwenye minyororo ya madeni ambayo imesababisha kudorora kwa masomo kwenye taasisi hizo.
Akizungumza kwenye hafla ya kutawazwa kwa chansela wa chuo kikuu cha Cooperative Dokta William Chitunga, Rais Ruto amekariri kujitolea kwa serikali yake kuimarisha vyuo vinavyokumbwa na changamoto za kifedha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































