VIONGOZI WA IGAD WAKUTANA NAIROBI KUJADILI NJIA ZA KUKABILI ATHARI ZA UKAME
Wataalamu kutoka sehemu mbali mbali bara la afrika wamekutana jijini Nairobi ili kujadili njia za kukabili athari za ukame katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na wataalamu 150 kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), ili kuimarisha ushirikiano katika kuboresha uwezo wa kukabiliana na maafa ya ukame katika maeneo kame.
Naibu katibu mtendaji wa IGAD, Mohamed Ware, amesema kuwa watu wa jamii za mpakani, wengi wao ni wafugaji na wakulima, ambao wanategemea mvua
Kutokana na kukosekana kwa miundombinu katika maeneo ya mpakani, juhudi za kibinadamu na misaada mara nyingi ni chache na uchelewa mno kwa wahanga.
Hata hivyo,Ametoa wito kwa eneo hilo kutekeleza mifumo thabiti ya tahadhari za mapema ili kuboresha uwezo wa kutabiri na kukabiliana na majanga ya ukame.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































