FAMILIA YAFURUSHA POLISI MWEA

Wakazi wa Mwea kaunti ya Kirinyaga wamepatwa na mshangao baada ya kituo cha polisi cha Riandira kufungwa na maafisa wote 6 wa polisi waliokuwa wakihudumu kituoni humo kuhamishwa kuhusiana na malimbikizi ya shilingi milioni 2 za kodi.
Maafisa hao wamefuurushwa na familia ya mfanyabiashara Mwangi Thuita aliyewataka waanze kulipa kodi kabla ya kifo chake mnamo mwaka wa 2018, baada ya kuwaruhusu waishi bure tangu mwaka wa 2016.
Hata hivyo, kamanda wa polisi wa Mwea West Rashid Ali amewahakikishia wakazi usalama, akisema doria itaendelea kushikwa na maafisa wa kituo cha Rukanga.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa