MAPEPO YA NHIF YAIHANGAISHA SHA
Changamoto za ufisadi zilizokuwa zikiikabili bima ya zamani ya afya NHIF zimeendelea kuikabili bima mpya ya SHA, serikali ikilaghaiwa takribani shilingi milioni 100 kupitia ulaghai unaoendelezwa kupitia ushirikiano wa hospitali na wagonjwa.
Kulingana na ripoti, hospitali zimekuwa zikighushi maelezo ya wagonjwa na kudai malipo mara mbili, waziri wa afya Aden Duale akitangaza kufunga zaidi ya hospitali 35 ambazo zimetajwa kwenye ripoti hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































