#Football #Sports

FRANCE WATOKA SARE NA CANADA.

Timu Ya Taifa Ya Ufaransa Imetoka Sare Tasa Na Canada Katika Mechi Ya Kirafiki Huku Mataifa Hayo Mawili Yakihitimisha Maandalizi Yao Ya Euro 2024 Na Copa America.

Ilikuwa Ni Mara Ya Mwisho Kwa Mshambuliaji Wa Ufaransa Na Mfungaji Bora Olivier Giroud Kucheza Katika Ardhi Ya Nyumbani Baada Ya Kutangaza Kustaafu Soka Ya Kimataifa Baada Ya Michuano Ya Ulaya, Na Alipokea Shangwe Kubwa Huko Nouveau Stade De Bordeaux.

Ufaransa, Ambao Waliilaza Luxembourg 3-0 Siku Ya Jumatano, Ni Miongoni Mwa Timu Zinazopewa Nafasi Kubwa Ya Kushinda Taji La Ulaya Huku Michuano Hiyo Ikianza Nchini Ujerumani Siku Ya Ijumaa.

Ufaransa Itamenyana Na Austria Katika Mechi Ya Kwanza Ya Michuano Hiyo Kabla Ya Kuvaana Na Uholanzi Juni 21 Na Poland Siku Nne Baadaye.

Canada, Chini Ya Kocha Mpya Jesse Marsch, Wataanza Copa America Dhidi Ya Argentina Ya Lionel Messi Mnamo Juni 20, Kabla Ya Kumenyana Na Peru Siku Tano Baadaye Na Chile Juni 29.

Imetayarishwa na Nelson Andati.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *